Monday, September 16, 2013

SHINYANGA BALOZI WA CHINA ANATAFUTA NINI?

Napenda kutoa dukuduku langu juu ya ziara ya Katibu Mkuu wa Ccm Mkoani Shinyanga,
Kwa upande wangu Aliweiwei sijafurahishwa wala kuridhishwa na ziara ya ndugu kinana na balozi wa China,hiyo ni ziara ya kichama  wala si yawawekezaji nchini.

 Balozi huyu anapokinadi chama cha Mapinduzi na kuvaa sare za ccm  inaimanisha nini? kwa wananchi wa shinyanga kwa ujumla, Nijuavyo balozi wa nchi huwakilisha nchi yake, Mahusiano bora kati ya nchi na nchi lakini si wawakilishi wa vyama vyao nchini  na hawapaswi kushiriki mambo ya siasa katika nchi husika , bali wanatakiwa kulinda masilahi na uhusiano baina ya nchi zao na kudumisha haki za binadamu na uhuru wake.
Wanashinyanga yawapasa muwe macho kwa  njama na mbwembwe za ccm zinazowachota kiakili ili mje kukichagua tena kwa kutumia danganya toto ya balozi  wa uchina,.napenda kuwajulisha kuwa watambueni Ccm kwa matendo yao ya rushwa, wizi wa kura , mmomonyoko wa maadili kwa serikali wanayoiongoza na kutolinda uhuru na mali za watanzania,  hawana jipya zaidi ni kutupora raslimali zetu kwa mgongo wa uwekezaji.